Na Sylvia Mwehozi
Shughuli za uchimbaji wa mafuta na gesi ni moja ya sekta ambazo zinakua kwa kasi katika nchi kadhaa barani Afrika ambazo zimegundua uwepo wa nishati hiyo.
Ghana ni mojawapo ya nchi ambayo imeanza shughuli za uzalishaji miaka mitano
iliyopita. Mkoa wa Magharibi ambao upo
kilometa 182 kutoka mji mkuu wa Accra ndiko shughuli za uchimbaji zinafanyika.
Hivi karibuni nilitembelea wilaya ya Sekondi-Takoradi iliyoko
mkoani humo na kufika katika eneo ambalo Gesi inazalishwa, ambapo kwa mujibu wa
wakazi wa mji huu , kumekuwa na
mabadiliko ya shughuli za kiuchumi, mwingiliano mkubwa wa watu wa kutoka sehemu
tofauti na kuibuka kwa fursa mbalimbali.
Suala la Idadi ya watu wanaokimbilia katika mkoa wa Magharibi nchini Ghana kutokana na kuwepo kwa
shughuli za uchimbaji wa gesi na mafuta, imezidi kuongezeka na kuleta wasiwasi
kwa wenyeji lakini pia ikihatarisha kudidimia kwa sekta nyingine za uzalishaji
ikiwemo sekta ya kilimo.
Kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2010 , mkoa
huo ulikuwa na wakazi laki mbili lakini hivi sasa idadi hiyo imezidi kuongezeka
na kufikia wakazi laki tano. Idadi hiyo inatajwa kuongezeka kwa sababu ya
kuanza kwa shughuli za uchimbaji wa gesi , ambazo zimeibua fursa nyingine, kama
ongezeko la ajira , na shughuli nyingine za kiuchumi.
Katika mazungumzo na ujumbe wa waandishi wa habari , Naibu
waziri wa mkoa huo Paul Evans Aidoo anasema kuwa wasiwasi umekuwa mkubwa kwa
sababu mkoa huo wa Magharibi ndo kitovu cha uchumi wa nchi kwa hivi sasa. ‘Kutokana
na ugunduzi wa gesi na mafuta, watu wengi kutoka kaskazini mwa mkoa huu
wanashuka chini, eneo la pwani, kwa kufanya hivyo tunahofia kuwa sekta nyingine
kama kilimo zitakufa’ alimalizia naibu waziri Aidoo ambaye pia anakaimu umeya
wa mkoa huo. Kwa mujibu wa kiongozi huyo, tayari kumeanzishwa mpango mkakati
ambao utawasaidia wananchi kuelewa umuhimu wa kushiriki katika uzalishaji wa
sekta nyingine badala ya kukimbilia mkoa huo kwa sababu ya mafuta.
Naibu Waziri wa mkoa wa Magharibi nchini Ghana , Amos
Anyimadu akizungumza na baadhi ya wandishi wa habari walipomtembelea ofisini
kwake.
Kauli yake inaungwa mkono na Amos Anyimadu, mwanazuoni na mtaalamu
wa masuala ya siasa , Kwanza anadiriki kusema kuwa wananchi walikuwa na matarajio
makubwa baada ya ugunduzi wa gesi na mafuta, hata hivyo matarajio hayo
yanapingana na uhalisia uliopo na hii inachangiwa na sababu kubwa ya kuiona
sekta hiyo ya gesi kama mkombozi pekee wa uchumi. ‘’Vyombo vya habari vinapaswa
kufanya kazi yake ipasavyo, kama nilivyowaambia mara ya kwanza ilikuwa mwaka
2009 wakati nilisikia kwenye radio moja kuwa Takoradi sasa ni mji wa mafuta, na
kulikuwa na mabango kadhaa, yanayosema karibu! Karibu! mji wa mafuta Takoradi
lakini nyie wenyewe mmetembea mmejionea hali ilivyo ’’ alisema Dr. Anyimadu.
Kwa mujibu wa mwanazuoni huyo, wananchi wanapaswa kuelimishwa
kuwa sekta ya mafuta na gesi pekee haviwezi kuwa chanzo cha mapato na kuacha
shughuli nyingine za kiuchumi.
Mtambo wa uzalishaji
gesi wa Atuabo ulioko mkoa wa magharibi nchini Ghana
Moja ya mikakati ambayo imeanzishwa na serikali ya mkoa huo
ni uanzishwaji wa taasisi ya Western Region coast foundation ambaye inalenga kuwa
jukwaa la wadau wote wa mafuta, na gesi pamoja na wananchi kujadili mahitaji ,
fursa , changamoto na kuwezesha upatikanaji wa majibu juu ya mahitaji hayo.
Tangu kuanzishwa kwake majadiliano katika jumla ya jamii 177
yamefanyika na masuala 620 yakiibuliwa katika Nyanja za uchumi, afya, maji,
elimu, miundombinu, mazingira na utawala bora. Wananchi wa eneo hilo wanasema kuwa fursa
zipo, hata hivyo wazawa wenyewe hawajawa tayari kuzitumia na matokeo yake
wanaishia kulalamika kuwa wageni wanazichukua. Sylvia Ousu ni mwanamke
mfanyabiashara katika eneo la market circle, anasema mwanzoni walikuwa na mategemeo
makubwa waliposikia gesi, lakini sasa ni tofauti, biashara haiendi kwasababu
watu wanalalamika hawana hela.
Hata hivyo anasema watu wanapaswa kuchangamkia fursa, ‘’ingawa
fedha hakuna , lakini kama sisi wanawake tunapaswa kufanya kazi , kama hapa sokoni
wanawake wengi wanafanya biashara , ni vizuri kuliko kutofanya kazi kabisa’’.
Mkoa wa magharibi sasa umekuwa lulu miongoni mwa maeneo ya
uwekezaji nchini Ghana, gharama za maisha nazo zimezidi kupanda , kwa mfano
chupa moja ya maji ya kunywa unaweza kuipata kwa cede 4 hadi 5 ambayo ni sawa
na dola 1.4 moja ya marekani tofauti na hali ilivyo mji mkuu wa ACCRA ambako chupa
ya maji unainunua kwa cede 1 hadi 2 sawa na dola 0.57 ya Marekani.
Tanzania ikiwa imeanza shughuli za uchimbaji inapaswa
kujifunza kuwa wananchi wanahitaji elimu ya kutosha ya kuzingatia mchango wa
sekta nyingine za kiuchumi badala ya kukimbilia mjini Mtwara pekee wakiwa na
matarajio ya kupata ajira, na fursa nyinginezo na hivyo kuhatarisha uchumi kwa
kuwa sekta nyingine zitakuwa hazizalishi